MWALIMU MKUU AACHIWE

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Islamic Byamungu, Kagera, ambaye anashikiliwa baada ya wanafunzi 10 kufariki kwa ajali ya moto.

Amesema kumshikilia wakati uchunguzi ukiendelea ni kumuongezea uchungu zaidi 

“Nafahamu Mkuu wa Shule iliyoungua Kyerwa ameshikiliwa na Polisi, ningeomba Polisi wakati uchunguzi unaendelea Mkuu wa Shule wamuachie ili wadhibiti na kujua kama ilikuwa ni ajali kweli au palikuwa na uzembe,hata akiwa nje atashirikiana na Polisi”.

“Kutokana na msiba uliotupata Kyerwa nizihimize Mamlaka husika ikiwemo Wizara ya Elimu na TAMISEMI zihakikishie shule zinazingatia usalama na Sheria kabla na baada ya kuanzishwa, hasa ukaguzi, ili madhara ya moto na ajali mashuleni zisijirudie”-JPM

SIMBA DHIDI YA BIASHARA MARA JUMAPILI

Kikosi cha simba kimerejea dar es salaam kujiandaa na mchezo wa tatu wa ligi kuu dhidi ya Biashara Mara utakaopigwa siku ya jumapili majira ya saa moja za jioni.

UCHAGUZI 2020


 KITAELEWEKA 2020 NANI KWENDA IKULU